Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utashi wa kisiasa umeleta mabadiliko kwa wanawake:AAWORD

Utashi wa kisiasa umeleta mabadiliko kwa wanawake:AAWORD

Utafiti uliofanywa na shirika moja nchini Kenya linalohusika na tafiti za maendeleo, AAWORD umebaini mafanikio makubwa pindi serikali inapojizatiti kuwezesha na kuwapatia fursa wanawake.

Afisa kutoka shirika hilo la wanawake, Juliette Gathoni-Kimemiyah ambaye yuko New York kuhudhuria mkutano wa 59 wa kamisheni kuhusu hali ya wanawake ametolea mfano sera ya kuhakikisha asilimia 30 ya zabuni zote za umma zinapatiwa wanawake.

Ameiambia idhaa hii kuwa sera hiyo imetoa fursa kwa wanawake wengi kutoa huduma kwa umma na kwamba utaratibu uliowekwa unahakikisha wanashiriki.

(Sauti ya Juliette)

Kwa mujibu wa utafiti wa AAWORD wanawake walioshiriki kwenye zabuni za umma walipata jumla ya shilingi bilioni 29 za Kenya lakini kulikuwa na changamoto ndani ya mafanikio kwa kuwa wengi nusu ya wanufaika walikuwa ni wanawake ambao tayari walikuwa na uwezo na hivyo serikali ikaweza utaratibu.

(Sauti ya Juliette)

Kwa mujibu wa Juliette, mtaala wa mafunzo kupitia mfuko wa UWEZO ni chachu ya mafanikio kwani mafunzo yanalingana na mazingira mathalani mijini na vijijini.