Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majadailiano ndiyo mwaruabini wa machafuko Yemen: OHCHR

Majadailiano ndiyo mwaruabini wa machafuko Yemen: OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu  ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) imesema inafuatilia hali ya mkwamo wa majadiliano ya kutafuta suluhisho kufuatia machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini Yemen kwa miezi kadhaa sasa.

Ofisi hiyo imetaka majadiliano kutumika ili kuikwamua nchi hiyo katika maandamano, ukamataji kuinyume na sheria, uwekwaji vizuizini na kuuwawa kwa wanahabari ikiwa ni sehemu ya matukio ya hivi karibuni nchini humo.

Ravina Samdashani ni msemaji wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva..

(SAUTI)

Tunawahimiza wahusika kuwa na mazungumzo yenye tija ili kuepuka migogoro zaidi. Hadi sasa, hakuna uchunguzi wa kina ulioanzishwa kuhusu ukiukwaji huo ambao unachochea ukosefu wa muda mrefu wa uwajibikaji wa vitendo hivyo katika miaka ya hivi karibuni.