Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazungumzia kukamatwa kwa Rais wa zamani wa Maldives

UM wazungumzia kukamatwa kwa Rais wa zamani wa Maldives

Umoja wa Mataifa umesema una taarifa za kukamatwa na kuwekwa korokoroni kwa Rais wa zamani wa Maldives Mohammed Nasheed na umesema unafuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini humo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaambia waandishi wa habari kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Maldives  Dunya Maumoon Jumatatu amempigia simu na Naibu Mkuu wa masuala ya siasa ndani ya Umoja huo Jens Toyberg-Frandzen .

 (Sauti ya Dujarric)

“Bwana Toyberg Frandzen amesisitiza umuhimu wa kuzingatia na kuheshimu taratibu zote kimahakama na kisheria dhidi ya Rais huyo wa zamani Nasheed.”

Bwana Dujarric amesema halikadhalika ametoa rai kwa serikali ya Maldives kuwa na kuruhusu mchakato wa wazi wa kisiasa na mashauriano na vyama vya upinzani ili kutoa fursa ya utulivu wa kudumu nchini humo.