Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na SIB zaungana kudhibiti magonjwa ya ndege na wanyama

FAO na SIB zaungana kudhibiti magonjwa ya ndege na wanyama

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeteua taasisi ya taarifa za kibaiolojia  cha Uswisi, SIB kuwa kituo cha kupata taarifa za teknolojia za kisasa zaidi za kukabiliana na magonjwa ya wanyama yanayoambukiza.

Miongoni mwa magonjwa hayo hatari ni homa ya mafua ya ndege na ule wa miguu na midogo unaopata wanyama wafugwao na wanyama pori.

Afisa Mkuu wa mifugo wa FAO Juan Lubroth amesema kupitia ushirikiano na FAO wataalamu wa SIB wameweza kutengeneza mbinu ya kuimarisha mfumo wa kubaini magonjwa mapema ya kuku na mifugo na kuepusha magonjwa hayo kuvuka mipaka.

Amesema mbinu hizo mpya zitasaidia shirika hilo kuelewa vitisho vya kibaiolojia na hivyo kuwezesha nchi kuchukua hatua haraka za kinga dhidi ya wanyama na binadamu, halikadhalika mazingira.

Kwa mujibu wa FAO, SIB ina kompyuta na programu za kisasa ambazo zina uwezo mkubwa wa kufuatilia magonjwa ya wanyama ikitolea mfano homa ya mafua ya ndege ambayo pia inaweza kumpata binadamu.