Ban akaribisha tangazo la Marekani kuhusu udhibiti wa gesi chafuzi

Picha@UNFCCC
Hewa chafuzi kutoka mitambo kama hii inasababisha uchafuzi wa hali ya hewa.

Ban akaribisha tangazo la Marekani kuhusu udhibiti wa gesi chafuzi

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Wakati maandalizi yanaendelea ya mkutano kuhusu mabadiliako ya tabianchi utakfaonyika mwezi Septemba mwaka huu mjini New York, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha tangazo la Marekani la kudhibiti kiwango cha gesi chafuzi zinazotolewa kwenye mitambo yake ya kuzalisha nishati

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric amesema tangazo hilo limetolewa na Rais Barack Obama mwishoni mwa wiki na amemkariri Ban akisema kuwa ni hatua muhimu katika kupunguza kiwango cha gesi chafuzi duniani zinazotishia afya ya binadamu, ukuaji endelevu wa uchumi na maendeleo. Hivyo ametoa wito..

(Sauti ya Dujarric)

Katibu Mkuu amesihi nchi zote kuchagiza jitihada zao za kupunguza utoaji wa gesi hizo na kuimarisha mikakati ya kwenda na mazingira na kukabiliana na kukabiliana na mabadiliko hayo. Ametoa wito kwa viongozi wa dunia kutumia fursa ya kipekee ya mkutano alioitisha mwezi Septemba mwaka huu kwa kutangaza hatua za kijasiri watakazochukua kitaifa au kikanda ili kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.”

Hatua hiyo ya Rais Obama pia imeungwa mkono na Christiana Figueres ambaye ni Katibu Msimamizi wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC.