Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi Uganda na wito kwa wakimbizi:

Polisi Uganda na wito kwa wakimbizi:

Katika jitihada za kuhakikisha usalama wa wakimbizi na jamii zinazowahifadhi, polisi nchini Uganda wametahadharisha wakimbizi kuhakikisha wanasajiliwa kabla ya kujichanganya na weneyeji.

Akizungumza na mwandishi wetu John Kibego, Kamanda wa polisi wa eneo la Ziwa Albert Charles Sebambulidde amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na ongezeko la matukio ya uhalifu yanayohusisha wakimbizi huko Bweyale mji ulio kilomita mbili kutoka kambi ya Kiryandongo inayohifadhi wakimbizi wengi kutoka Sudan Kusini.

(Sauti ya Charles Sebambulide)