Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Somalia yaridhia Mkataba wa Haki za Mtoto wa UM

Serikali ya Somalia yaridhia Mkataba wa Haki za Mtoto wa UM

Huku dunia ikiingia miaka ya 26 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Haki za Mtoto, Somalia imekuwa nchi ya 194 kuridhia Mkataba huo, na hivyo kuweka bayana azma yake ya kuboresha maisha ya watoto.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake amesema, kwa kuridhia mkataba huo, Somalia imewekeza katika ustawi wa watoto wake, na hiyo mustakbali yao.

Christophe Boulierac ni Msemaji wa UNICEF mjini Geneva.

(SAUTI Christophe Boulierac )

UNICEF iko tayari kuisaidia serikali ya Somalia ili kutafsiri haki za watoto katika vitendo kwa ajili ya watoto wa nchi hiyo. Nawakumbusha kwamba Somalia ni moja ya sehemu hatari zaidi duniani kwa watoto. Mtoto mmoja kati ya saba anakufa kabka ya kufikia umri wa miaka mitano, wengi kwa sababu ya magonjwa yanayoweza kuzuiliwa. Watoto wanne tu kati ya kumi wanaenda shuleni, na takwimu ni mbaya zaidi kwa wasichana”

Kwa upande wake, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay, amesema anakaribisha kuridhiwa kwa Mkataba wa Haki za Mtoto na Somalia, huku akisema hii ni hatua muhimu ya kulinda na kukuza haki za watoto wote nchini Somalia.