Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkwamo vikubwa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto, repoti Mpya ya UM kuhusu Watoto katika mgogoro wa Sudan Kusini

Mkwamo vikubwa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto, repoti Mpya ya UM kuhusu Watoto katika mgogoro wa Sudan Kusini

Ripoti ya kwanza ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na mgogoro wa kutumia silaha Sudan Kusini iliyochapishwa leo inamesema mgogoro nchini humo umeleta mkwamo mkubwa kwa ajili ya ulinzi wa watoto.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mgogoro huo ulioanza mwaka mmoja uliopita umepelekea kushuhudiwa ukiukaji mkubwa wa haki za watoto kati ya mwezi Machi mwaka 2011 na mwezi Septemba mwaka 2014.

Ripoti inasema madhila hayokwa watoto yanafuatia miaka miwili ya kuongezeka kwa macahfuko baada ya kuzuka kwa vita.

Halikadhalika, ripoti inasema kwamba idadi ya matukio ya ukiukwaji mkubwa uliotekelezwa dhidi ya watoto kutoka katikati ya Desemba 2013 na Septemba 2014 ni kubwa zaidi kuliko mwaka 2012 na 2013 pamoja.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu watoto na migogoro ya silaha, Leila Zerrougui, amesema taarifa zilizokusanywa na kuthibitishwa na Umoja wa Mataifa ni za kutisha huku akisema watoto wa Sudan Kusini hawakuathiriwa na ghasia pekee, bali, wamekuwa walengwa wa moja kwa moja na pande zote katika mgogoro.