Ebola hukera jamii, lazima kuitokomeza: Banbury

30 Disemba 2014

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola UNMEER Anthony Banbury amesema Ebola ni ugonjwa unaokera na hivyo ni  lazima kuutokomeza kwa mikakati maalum. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya

(TAARIFA YA GRACE)

Akizungumza muda mfupi baada ya kukamilisha ziara yake nchini Liberia ambako alikutana na viongozi kutathimini hatua za kutokomeza homa ya Ebola, mkuu huyo wa UNMEER amesema serikali imepiga hatua muhimu lakinia akasisitiza.

(SAUTI BANBURY)

Tunahitaji kuimarisha uwezo wetu na muhimu sana ni kwamba tuna ufauatiliaji mzuri kwahiyo tunaweza kugundu amapema ikiwa kuna mlipuko. Tunahitaji mkakati wa wilaya kwa wilaya tunahitaji kuwepo mashinani kwa hakika.

Kadhalika Banbury amewataka watu wa Liberia kuwa imara licha ya madhila waliyokutana nayo ikiwamo kuwapoteza wapendwa wao akisema kuwa Umoja wa Mataifa uko nao katika kuhakikisha janga hilo linatoweshwa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud