Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njugumawe ni lishe tosha:FAO

Njugumawe (Picha@FAO)

Njugumawe ni lishe tosha:FAO

Njugumawe, aina ya maharagwe yanayolimwa sana kwenye za nchi Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara ndio zao la asili kwa mwezi huu wa Disemba. Ripoti kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO linasema njugumawe zao asili kwenye eneo hilo linastawi kwenye maeneo kame na hata udongo usio na rutuba ya kutosha.

Kwa upande wa lishe njugumawe ina asilimia 63 ya wanga, asilimia 19 protini na asilimia 6.5 mafuta na inaweza kuchemshwa na kuliwa kama kitafunwa ikiwa mbichi au kuchemshwa baada ya kukauka.

Tovuti  ya FAO inaelezea mapishi ya njugumawe ikisema unga wake unaweza kutumika kutengeneza maandazi, keki au biskuti na majani yake ni lishe bora kwa mifugo.