Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miradi ya Benki ya dunia ijali haki za binadamu: Mtaalamu

Philip Alston, Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Devra Berkowitz)

Miradi ya Benki ya dunia ijali haki za binadamu: Mtaalamu

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya umaskini na haki za binadamu Philip Alston ameitaka Benki ya Dunia kuzingatia na kutambua haki za binaadamu wakati huu inapoaanda sera mpya kuhusu miradi. Taarifa kamali na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Sera hiyo ambayo ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai mwaka huu na kisha kusambazwa kwa umma kwa ajili ya kukifanyia tathmini itakuwa ikitumika na benki hiyo wakati wa utoaji fedha kugharimia miradi ya maendeleo.

Akizungumzia kuhusu misingi ya kuheshimiwa kwa haki za binadamu, mtaalamu huyo wa UN alisema kuwa ni vyema Benki ya Dunia ikazingatia jukumu kuu ambalo ni kuheshimiwa kwa haki za binadamu.

Katika barua yake kwenda kwa rais wa Benki ya Dunia, Philip amesema kuwa wakati huu kunapokusanywa michango toka kwa umma kwa ajili ya kuifanikisha sera hiyo mpya, itakuwa jambo lisilo na maana iwapo misingi ya kuheshimiwa kwa haki za binadamu litapuuzwa.

Kumekuwa na ongezeko la malalamiko kutokana na kile kinachoelezwa kwamba mapendekezo yaliyopo kwenye sera hiyo mpya hayatoi mwelekeo halisi kuhusu kulinda na kuheshimiwa kwa haki za binadamu huku wengine wakienda mbali zaidi wakisema kuwa sera hiyo haijakidhi viwango vya kimataifa.