Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitendo vya mauaji vyaongezeka:Ripoti

Vitendo vya mauaji vyaongezeka:Ripoti

Utafiti mmoja wa kimataifa ambao unahusiana na hatua zinazochukuliwa kuzuia vitendo vya unyanyasaji duniani umesema kuwa kiasi cha watu 475,000 waliuawa katika kipindi cha mwaka 2012 huku wengi wao wakiwa na watu wenye umri wa kati ya miaka 15-44. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Ripoti hiyo iliyotolewa leo mjini Geveva Uswisi imesema kuwa pamoja na vitendo vya mauaji kupungua kwa asilimia 16  katika kipindi cha mwaka 2000 na 2012 lakini hata hivyo vitendo vya unyanyasaji bado vimeendelea kuwa tishio duniani.

Ripoti imeyataja makundi ya kina mama na watoto kuwa ndiyo waathirika wakumbwa wa matukio ya kunyanyaswa na kufafanua kuwa kila kwenye watoto wanne basi mmoja wao amekubwa na matukio hayo.

Ripoti hiyo ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwamo lile la afya duniani WHO na shirika la maendeleo UNDP imezitaaka taasisi zinazohusika kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hiyo.