Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili hali nchini Liberia na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Herve Ladsous akihutubia Baraza la Usalama(Picha ya UM/Eskinder Debebe/maktaba)

Baraza la usalama lajadili hali nchini Liberia na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa  hii leo limekuwa na mashauriano kuhusu hali nchini Liberia pamoja na Jamhuri ya Afrka ya Kati CAR. Grace Kaneiya amefuatilia mkutano huo(TAARIFA YA GRACE)

Mkutano huo umeanza kwa kupigia kura azimio la kuendeleza vikwazo dhidi ya Liberia  vinavyofikia ukomo tarehe 12 mwezi huu wa Desemba. Azimio hilo liliungwa mkono na kupitishwa.

Kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR baraza la usalama limejadili hali ya kibinadamu na madhara ya machafuko ambapo mkuu wa  operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema..

(SAUTI LADSOUS)

Ladsous amesema kwa ujumla hali ni mbaya bado nchini humo lakini ujumbe wa Umoja wa Matifa nchini humo MINUSCA unajitahidi kusaidia kurejesha amani na kurejesha Amani.