Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumepiga hatua dhidi ya Ebola, tusibweteke:Nabarro

Tumepiga hatua dhidi ya Ebola, tusibweteke:Nabarro

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya homa ya ebola Dk, David Nabarro amesema kuwa hatimaye sasa dunia inaweza kujisifikia imepata mahali kwa kupumua kutokana na namna ilivyoweza kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa ebola.Hata hivyo ameeleza kuwa bado kuna kazi kubwa iliyombele. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Sauti ya George)

Mtaalamu huyo amesema kuwa kwa kuangalia hali ilivyo kuna matumaini na kwamba tangu mwezi Septemba mwaka huu nchi za Afrika magharibi ambazo ziliathiriwa pakubwa na homa hiyo sasa zimepata ahueni.

Lakini hata hivyo alionya kuwa virusi vya homa hiyo bado vinaendelea kuwaandamana wananchi hasa huko Sierra Leone na maeneo mengine ya mbali ya kaskazini mwa Guinea.

Alishutumu hatua ya kukosekana kwa matibabu inayojitokeza katika baadhi ya vituo nchini Sierra Leone lakini akaonyesha matumaini yake kwa kusema kwamba wakati wote maeneo hayo yanaweza kufikiwa na huduma muhimu ikiwamo vitanda.

"Hatuwezi kukaa nyuma na kusema kwamba kazi kwa kiasi kikubwa imekamilika kutokana na kujitokeza kwa maambukizi madogo ambayo yanaweza kusambaa kwa haraka na hata kufika katika maeneo ambayo kwa sasa kiwango cha maambukizi yake ni sifuri."