Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya kimbari yanaepukika tukichukua hatua: Dieng

Adama Dieng.(Picha ya UM/Jean-Marc Ferré)

Mauaji ya kimbari yanaepukika tukichukua hatua: Dieng

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia muaji ya kimbari  Adama Dieng  amesema mauaji hayo sio kitu kinachatokea ghafla kwahiyo yanaweza kuzuilika.

Akiongea na waandishi wa habari mjini  New York ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya maadhimisho ya mkataba wa mauaji ya kimbari uliopitishwa mwaka 1948 , Bwana Dieng amesema mauaji ya kimbari ni mchakato na hivyo ikiwa hatua za usitishaji zitachukuliwa mapema mauaji hayo yanaepukika na hivyo

(SAUTI DIENG)

"Lazima tukubali kuwa hakuna sehemu ya ulimwengu ambayo inaweza kujihesabu kuwa na kinga dhidi ya hatari ya mauaji ya kimbari. Kutokana na hilo kanda na mataifa yote lazima yajenge uwezo dhidi ya uhalifu huu ikiwa ni Kaskazini, kusini, mashariki au Magharibi."

Waandishi wa habari walitaka maoni yake kuhusu maamuzi ya Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC dhidi ya rasi wa Kenya Uhuru Kenyatta mshauri huyo maalum wa Katibu Mkuu akafafanua

(SAUTI DIENG)

"Tunaheshimu uhuru wa ICC na pia uamuzi wake. Nakubali kuwa uwajibikaji dhidi ya uvunjaji wa haki za binadamu nchini Kenya ni muhimu , na ni muhimu kupatia majibu matakwa ya waathirika . Kuana maelfu ya waathirika wanaotarajia haki ya kisheria itekelezwe na pia lazima tuwawajishe wahusika wa viendo uhalifu huu uliotendeka."