Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaume walionusurika Ebola wanawaambukiza wake zao- mtaalam wa WHO

WHO/C. Black — in Sierra Leone.
Picha:

Wanaume walionusurika Ebola wanawaambukiza wake zao- mtaalam wa WHO

Mshauri wa Shirika la Afya Duniani, WHO nchini Liberia ameripoti kuwepo idadi kubwa ya wanawake kuambukizwa kirusi cha Ebola na waume zao ambao ni manusura wa homa hiyo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace Kaneiya)

Dkt. Anne Atai Omoruto, mtaalam wa afya kutoka Uganda ambaye yupo kwenye kituo cha matibabu cha Island Clinic mjini Monrovia, amesema kwamba wamekuwa wakiona idadi kubwa ya wake za wanaume walionusurika Ebola wakija kwenye kituo hicho wakiwa wameambukizwa kirusi cha Ebola.

Amesema sababu ya hali hii ni kwamba wanaume manusura wa Ebola hawatumii mipira ya kondomu pale wanapojamiiana na wake zao.

Amesema kwamba kawaida, wanawashauri wanaume waliopona kutokana na kirusi cha Ebola kujiepusha na vitendo vya ngono au kutumia kinga ya mipira ya kondomu, lakini inaonekana kwamba hawafuati maagizo hayo kwani wake zao wanaendelea kuwasili kwenye kituo cha matibabu.

Katika mahojiano na Olive Thomas wa Redio ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, UNMIL, Bi Atai amesema..