Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICN2 ni ishara ya nchi kujizatiti kuondokana na lishe duni: Ban

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu lishe ndio umeaaza na hii ndiyo moja ya nembo zake ikisisitiza mlo. (Picha:UN/Stéphanie Coutrix)

ICN2 ni ishara ya nchi kujizatiti kuondokana na lishe duni: Ban

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu lishe umeanza huko Roma Italia ambapo Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema ni fursa mpya ya kutokomeza njaa na utapiamlo duniani . Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ujumbe wa Ban aliuwasilisha kwa njia ya video ambapo amesema hatua kubwa imefikiwa tangu aanzishe changamoto ya kutokomeza njaa duniani iliyoleta pamoja serikali, taasisi za kiraia na sekta binfasi.

Amesema hadi sasa zaidi ya mataifa 100 barani Afrika, Amerika Kusini na Caribbean yameazimia kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2025, kama walivyoahidi mataifa mengine ya  Asia, Pasifiki na Mashariki ya Kati huku akizungumzia mataifa yalienda mbali zaidi.

(Sauti ya Ban)

Mataifa hayo 54 yanayoongoza kwenye harakati ya kuimarisha lishe  yametambua kuwa lishe ni sehemu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Nchi nyingi zaidi zinachukua hatua ya kukabiliana na utipwatipwa. Napongeza serikali zilizofanikiwa kufanya mashauriano ya azimio la Roma kuhusu mfumo wa lishe.”

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni Waziri wa afya kutoka Uganda, Sarah Opendi.

(Sauti ya Waziri Opendi)

“Kilicho muhimu zaidi kwenye  ajenda yetu ni kuhakikisha tunatekeleza tunayosema. Tumetoa ahadi, na kuhakikisha kwamba hatujikiti kwenye usalama wa chakula pekee  bali pia kwenye chakula bora ambacho watu na watoto wetu wanakula, na hivyo kuwa na afya na maisha bora.”

Stéphanie Coutrix