Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vituo vya kutibu Ebola Sierra Leone vinazingatia viwango:UNICEF

Picha: © UNICEF/NYHQ2014-3008/James

Vituo vya kutibu Ebola Sierra Leone vinazingatia viwango:UNICEF

Harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola zinaendelea kila uchao wakati huu ambapo idadi ya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo ikiwa imefikia 5,177 kati ya wagonjwa 14,413 waliothibitishwa.

Miongoni mwa nchi zilizokumbwa zaidi ni Sierra Leone ambapo tangu ugonjwa ubishe hodi mwezi Mei mwaka huu zaidi ya watu Elfu Moja wamefariki dunia.

Hatua zinachukuliwa kusaidia nchi hiyo na hatua za hivi karibuni zaidi ni za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF ambalo limeamua kusogeza vituo vya matibabu karibu na wananchi.

Kufahamu kwa undani zaidi kuhusu hatua hiyo ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.