Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwezo wa Lebanon kupokea wakimbizi wa Syria umepungua: UNHCR

Familia wa wasyria wakijiandikisha kama wakimbizi, Halba kaskazini mwa Lebanon.© UNHCR/F.Juez

Uwezo wa Lebanon kupokea wakimbizi wa Syria umepungua: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limedhibitisha kupokelewa kwa wakimbizi wachache wa Syria nchini Lebanon ambayo imekuwa ikihifadhi kiasi cha wakimbizi milioni 1.17 ambao wamekimbia mapigano nchini mwao Syria.

Tangu kuripotiwa kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wakimbizi wa Syria nchini Lebanon UNHCR imesema kuwa kiwango cha wakimbizi hao waliorodheshwa kimepungua na kufikia 40,000 .

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari Lebanon haitizamwi tena kama taifa linalowapokea rasmi wakimbizi wa Syria isipokuwa tu kwa wale wenye mahitaji muhimu ya kibinadamu.

Hivi karibuni UHNCR iliitaka jumuiya ya kimataifa kuisaidia Lebanon kuboresha miundo mbinu yake kama vile shule, vituo vya afya ili kuliwezesha taifa hio kwenda sambamba na mahitaji halisi.