Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yaelezea mafanikio yake dhidi ya Malaria

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wa Tanzania, Dkt. Pindi Chana. (Picha:UN/Idhaa ya Kiswahili)

Tanzania yaelezea mafanikio yake dhidi ya Malaria

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu mpango mpya kwa maendeleo barani Afrika, NEPAD na ugonjwa Malaria.

Akifungua mjadala huo, Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa amesema mjadala huo ni fursa ya kipekee ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu ya Afrika kwa kuangalia mafanikio na changamoto.

Mathalani amesema vita dhidi ya Malaria imekuwa na mafanikio kwingineko lakini bado ni kitisho cha afya barani Afrika kwani asilimia 80 ya wagonjwa wa Malaria wako barani Afrika.

“Mafanikio yetu yasitufanye tupunguze kasi yetu. Ni lazima tuongeze juhudu maradufu dhidi ya Malaria na kufikia lengo la kutokomeza kabisa ugonjwa huu. Ni lazima kuendeleza azma na utashi wetu kuwa Malaria inazuilika na inatibika na inaweza kutokomezwa.”

Katika mkutano huo, Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Pindi Chana ambaye moja ya ujumbe wake mkuu ilikuwa mafanikio katika kukabiliana na malaria.

Punde baada ya hotuba yake alihojiwa na Idhaa hii na kueleza siri ya mafanikio hususan huko Tanzania Zanzibar.

(Sauti ya Pindi Chana)