UNHCR yaonya kuhusu kupuuza mahitaji ya wakimbizi Afrika

29 Septemba 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kuamka kuzuia kutoendelea kutokea mapigano hasa huko barani Afrika ambako zaidi ya watu milioni 16 wamekosa makazi kutokana na machafuko yanayojitokeza.

Shirika hilo limesema kuwa kuongezeka wa idadi ya wakimbizi kumezidisha mzigo wa kuwahudumia hasa wakati huu kunakojitokeza changamoto ya ukosefu wa fedha. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Akizungumza kwenye mkutano unawajumuisha maofisa wa ngazi za juu wanajadiliana kuhusiana hali ya wakimbizi barani Afrika, Kamishna wa UNHCR Antonio Guterres amesema kuwa kujitokeza kwa migongano ya mambo ikiwemo kujirudia kwa machafuko kumezidisha mzigo wa kuwakirimu wakimbizi hao.

Serikali nyingi pamoja na jumuiya zinazojitolea kuwasaidia wakimbizi hao zinakabiliwa na hali ngumu kwa vile tatizo la wakimbizi barani Afrika limeendelea kukua kutokana na kukosekana kwa utengamano wa mambo mengi.

Bwana Guterres alionya juu ya kile alichokiita kupuuzia suala la misaada ya kibinadamu barani Afrika kwa kusema kuwa hali hiyo inaweza kuzalisha majanga zaidi hapo baadaye. Aliitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia juhudi za kuwahifadhi wakimbizi hao.

(Sauti ya Guterres)

"Kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi katika kambi za hifadhi ni tishio kwa usaidizi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kwa mfano Wasomali na watu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na wakimbizi wengi walio barani Afrika ambao wamesahaulika na jamii ya kimataifa kwa mfano watu wa Eritrea na waDarfur na, Wasarawi na watu wa Ivory Coast ambao kurudi nyumbani kwao kwa hiari kuliathiriwa na mlipuko wa Ebola. Mchanganyiko wa changamoto mpya na mizozo ya awali ni mzigo mkubwa kwa nchi zinazowahifadhi wakimbizi na jamii na kwa UNHCR na wadau wake."

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter