Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afueni Sudan Kusini kufuatia kuimarika usalama wa chakula kwa muda

Picha: UN South Sudan(FAO)

Afueni Sudan Kusini kufuatia kuimarika usalama wa chakula kwa muda

Usaidizi wa kibinadamu unachangia pakubwa kubadilisha hali ya maisha nchini Sudan Kusini, imesema taarifa ya Shirika la Chakula na Kilimo, FAO. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Juhudi za pamoja za mashirika yanayohusika na usalama wa chakula na riziki yakiwemo FAO na Shirika la Mpango wa Chakula, WFP, pamoja na yale ya kuimarisha lishe, zimewanusuru watu wapatao milioni 2 kutokana na hatari ya njaa na uhaba mbaya mno wa chakula.

Licha ya kuboreshwa kwa hali ya usalama wa chakulakwa muda mfupi, watu wapatao milioni 1.5 wanatazamiwa kusalia katika hali mbaya ya kukosa hakikisho la chakula hadi mwishoni mwa mwaka huu 2014.

Idadi hii inatarajiwa kuongezeka wakati msimu wa kiangazi ukianza mapema mwakani, ambapo idadi ya watu watakaokuwa katika hali ya dharura ya ukosefu wa chakula inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50, hadi milioni 2.5.