Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yasaidia kupaza sauti ya mkunga Tanzania

Elvina-Mkunga Tanzania. Picha@UNFPA

UNFPA yasaidia kupaza sauti ya mkunga Tanzania

Uimarishaji wa afya ya uzazi ni lengo nambari tano katika malengo ya milenia ambayo yatafikia ukomo mwakani. Ili kutimiza lengo hili ni muhimu kuhakikisha kwamba watoa huduma wana vifaa vinavyohitajika na kwamba idadi ya watoa huduma, kama vile wakunga, inakwenda sambamba na walio na mahitaji.

Katika nchi zinazoendelea, bado lengo hili haliijafikiwa kikamilifu kwa sababu ya changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo wakunga.

Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala inayoangazia mkunga kutoka Tanzania.