Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na mapigano ya Gaza

UN Photo.
Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@

Ban asikitishwa na mapigano ya Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa bado anaingiwa na woga kuhusiana na hali ya mambo katika eneo la Gaza ambako amesema kuwa pamoja na mwongozo uliotolewa na Baraza la Usalama lililotaka usitishwaji mapigano, lakini hali imeendelea kuwa mbaya na siyo tu kwa raia wa Palestina lakini pia kwaWaisrael.

Katika taarifa yake Ban amesema kuwa kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili, kuna haja ya kuachana na mapigano na kuchukua duru mpya ya kuleta amani. Amesisitiza kuwa jambo hilo linapaswa

kutekelezwa sasa bila kukawia.

Amesema kuwa kitendo cha Hamasi kuvurumisha maroketi yake kuwalenga raia wasio na hatia wa Israel ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Ban amezungumzia pia hali ngumu inayowaandama mamia ya raia wa Israel ambao picha zao zinaonyesha jinsi walivyo kwenye hali ngumu wakitafuta hifadhi kujinusuru na makombora kutoka Palestina.

Katika upande mwingine ameelezea masikitiko yake kuhusiana na hali ya wasiwasi inayojitokeza kwa familia za Kipalestina kutokana na makombora yanayorushwa na vikosi vya Israel.

Kwa kuzungatia mazingira hayo Ban amesisitiza juu ya haja ya pande hizo kusitisha mapigano mara moja ili kunusuru maisha ya raia wa pande zote mbili.