Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Ethiopia na hofu kuhusu hatma yao

Wanawake wakirudi kwenye mahifadhi yao baada ya kupokea msaada wa chakula kutoka kwa WFP kwenye Yusuf Batil refugee Camp. Picha: WFP/George Fominyen

Wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Ethiopia na hofu kuhusu hatma yao

Nchini Sudan Kusini mapigano yaliyoanza tarehe 15 Disemba mwaka 2013 yamesababisha zahma kubwa kwa mamia ya maelfu ya raia kwani katika kusaka usalama wao wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Ethiopia.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa Ethiopia ndio yenye idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan Kusini na miongoni mwao ni kituo cha mpakani cha Burbe. Je hali yao iko vipi? na wana matumaini yapi? Basi ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.