Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe kutunza urithi wa dunia uliopo Tanzania: UNESCO

Picha@UNESCO/Ron Von Oers

Hatua zichukuliwe kutunza urithi wa dunia uliopo Tanzania: UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limetangaza kuingiza mbuga ya Hifadhi ya Wanyama ya Selous, nchini Tanzania, katika orodha ya Urithi wa Dunia ulio hatarini, kwa sababu ya ujangili uliosababisha idadi ya wanyamapori kupungua sana, hususan tembo.

Akiongea na idhaa ya redio ya umoja wa mataifa leo, Daktari Donatius Kamamba, ambaye ni.Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale, UNESCO Tanzania, amesema hii itasaidia kuchukua hatua:

(Sauti ya Kamamba)

Halikadhalika, sehemu ya Kilwa Kisiwani na magofu ya Songo Mnara yameondolewa kutoka orodha hiyo hiyo baada ya utunzaji na uboreshaji uliofanyika huo kulingana na vigezo vilivyowekwa na kamati ya urithi wa dunia. Huyu hapa tena Dkt Kamamba