Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili amani na usalama Afrika, Sahel yamulikwa

UN Photo/Marie Frechon
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu eneo la Sahel, Hiroute Guebre Sellassie(kushoto):

Baraza la Usalama lajadili amani na usalama Afrika, Sahel yamulikwa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili suala la amani na usalama barani Afrika, na kuhutubiwa na Mwakilishi Maalum mpya wa Katibu Mkuu kuhusu eneo la Sahel, Hiroute Guebre Sellassie, ambaye ameiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu ya tarehe 6 Juni kuhusu utekelezaji wa mkakati wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukanda huo. Taarifa kamili na Joshua Mmali

(Taarifa ya Joshua)

Ripoti iliyotolewa leo ndiyo ya kwanza kuwasilishwa na Bi Sellassie kwa Baraza la Usalama tangu alipoteuliwa kuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu eneo la Sahel.

Ripoti hiyo ya Katibu  Mkuu inatoa maelezo mapya kuhusu yaliyojiri katika ukanda huo tangu Julai 1 2013, na pia kuhusu utekelezaji wa mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusuSahel, ukijikita kwa masuala ya utawala, usalama na uhimili wa matatizo.

Akiiwasilisha ripoti hiyo, Bi Sellassie ameelezea kwa kifupi mikakati ya kikanda na shughuli za Umoja wa Mataifa zinazolenga kuimarisha uratibu miongoni mwa wadau mbali mbali wanaoutekeleza mkakati wa pamoja wa Sahel.

 

 

“Iwapo jamii ya kimataifa haitaboresha utaratibu wa majukumu yake, rasilmali chache zilizopo hazitakuwa na matokeo yanayotarajiwa. Kuchukua hatua haraka na kwa utaratibu ni muhimu, ili kukabiliana mwenendo wa sasa wa mizozo ya mara kwa mara, na kuelekea kwa mustakhbali wa utulivu na maendeleo katika ukanda huo.”