Kutoka Darfur, Lt. Kanali Ntahena azungumza kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani
Tarehe 29 Mei ni siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa duniani, kukumbuka wale waliofariki dunia wakihudumu na pia kutoa shukrani kwa wanaoendelea kutoa huduma hiyo sehemu mbali mbali duniani. Umoja wa mataifa una operesheni 16 za ulinzi wa amani duniani kote zikiwa na askari jeshi, polisi na watendaji wa kiraia wapatao 118,000. Umoja wa Mataifa hauna jeshi bali hupata watendaji hao kutoka nchi wanachama, miongoni mwa watendaji hao ni Luteni Kanali Furahisha Ntahena kutoka Tanzania ambaye ni Mratibu wa kitengo cha habari cha Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, Sudan, UNAMID. Katika kuzungumzia siku hii alihojiwa na Assumpta Massoi na hapa anaanza kwa kujibu ana lipi la kujivunia kwa siku hiyo adhimu.