Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ziwekeze katika ufugaji wa samaki ili kuinua sekta hiyo: FAO

@FAO/F. Cardia

Serikali ziwekeze katika ufugaji wa samaki ili kuinua sekta hiyo: FAO

Ripoti mpya ya Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO imesema sekta ya ufugaji wa samaki katika maji barini na baharini barani Afrika inaweza kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa uchumi iwapo serikali zitawekeza zaidi tofauti na sasa ambapo ufugaji huo ni wa kiwango kidogo na unatia hofu kwa walaji. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi

 (Taarifa ya Assumpta)

Alessandro Lovateli kutoka Idara ya samaki na ufugaji samaki ya FAO ameiambia idhaa hii kwa sasa sekta hiyo inakua lakini mchango wake katika soko la kimataifa inaweza kuwa kubwa zaidi iwapo…

(sauti ya Alessandro)

 "Kile tunachotaka kushuhudia pale ni kuanzishwa kwa teknlojia sahihi, na kuhakikisha kuwa ufugaji samaki unachukuliwa kama biashara. Tunahitaji kusaidia nchi kuanzisha miradi ya biashara badala ya miradi midogo ya vijijini. Hiyo miradi midogo inaweza kujumuishwa! Nchi zinapaswa kutambua kuwa kuna fursa ya kuanzisha ajira, chakula zaidi kwa wananchi na pia kwa kuuza nje ya nchi.”

AmetajaUgandakuwa mfano wa mafanikio ya ufugaji wa samaki aina ya Sato katika maji baridi ilhali Msumbiji iko mstari wa mbele katika ufugaji wa samaki aina ya Kamba baharini.

Amesema kuna hofu ya uharibifu wa mazingira katika ufugaji wa samaki aina ya kamba baharini hususan ukataji wa mikoko, lakini FAO hutoa mwongozo na ni vyema kuweka mizania.

(Sauti ya Allessandro)

"Tumeimarika sana  katika kipindi hiki cha miongo  mitatu na tumechukua hatua kubwa sana kudhihirisha kuwa ufugaji samaki unafanyika kwa misingi endelevu