Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo cha taarifa za UM chafunguliwa Tanzania Zanzibar

Kituo cha taarifa za UM chafunguliwa Tanzania Zanzibar

Kituo kipya cha vijana kimefunguliwa leo Tanzania Zanzibar kikiwa na lengo la kutoa taarifa kwa vijana kuhusu kazi za Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Mratibu wa vijana wa chama cha Umoja wa Mataifa vsiwani humo, Ame Haji, ufunguzi wa kituo hiki umetokea wakati muafaka kwa sababu vijana wa Zanzibar walikuwa wamebaki nyuma ukizingatia kwamba katika maeneo mengine ya Tanzania kama vile Dar es Salaam tayari vijana walikuwa wakipata taarifa za Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu.

Akizungumza na idhaa hii Bwana Haji amesema:

(SAUTI YA BWANA AME HAJI)