Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa utashi wa kisiasa wakwamisha mipango miji nchi zinazoendelea

Ukosefu wa utashi wa kisiasa wakwamisha mipango miji nchi zinazoendelea

Kikwazo kikubwa katika mikakati ya kuendelezea miji miongoni mwa nchi zinazoendelea ni ukosefu wa utashi miongoni mwa viongozi.

Akizunguzma katika mahojiano na Joshua Mmali wa idhaa hii mjini Medellin, Colombia kunakofanyika mkutano wa saba kuhusu mipango miji, mwakilishi wa serikali ya Kenya Suzan Araka amesema ukosefu wa utashi umesababaisha nchi zinazoendelea kushindwa kupiga hatua stahili licha ya kuhudhuria mikutano kadhaa kama huo.

(SAUTI SUSAN)

Hata hivyo Bi. Araka amesema serikali ya Kenya imechukua hatua ya kuendeleza miji katika majimbo 47 nchini humo.