Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza kuidhinishwa kwa MINUSCA huku akipongeza MISCA

Ban apongeza kuidhinishwa kwa MINUSCA huku akipongeza MISCA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa namba 2149 lililoanzisha ofisi ya kuimarisha ya kuimarisha utulivu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric amewaeleza waandishi wa habari kuwa Ban anaamini hatua hiyo muhimu itawezesha kuwapelekea wakazi wa nchi usaidizi wa haraka wanaohitaji.

Ban amesema aliguswa na ziara yake nchini humo tarehe Tano mwezi huu na kutoa wito kwa kusitishwa mara moja kwa mauaji ya raia wasio na hatia yanayolenga kundi Fulani na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu.

Hata hivyo ametoa pongezi..

(sauti ya Dujarric)

Katibu Mkuu anapongeza jitihada za kipekee za kikosi cha Afrika kinachoungwa mkono na jamii ya kimataifa, MISCA, ambacho kitaendelea na jukumu lake hadi tarehe 15 Septemba sambamba na askari wa Ufaransa, Sangari na wale walioidhinishwa hivi karibuni na Muungano wa Ulaya, EUFOR. Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na MISCA kuhakikisha mpito stahili kuelekea MINUSCA.”

Katibu Mkuu ametoa wito kwa wadau wote kuongeza usaidizi wao kwa MISCA hadi MINUSCA itakapoanza operesheni zake rasmi