Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2013 ni miongoni mwa 10 iliyokuwa na joto kali zaidi:WMO

Mwaka 2013 ni miongoni mwa 10 iliyokuwa na joto kali zaidi:WMO

Mwaka 2013 ulikuwa miongoni mwa miaka iliyokuwa na joto kali saana tangu kuanza kuwekwa kumbukumbu ya wiwango vya joto mnamo mwaka 1850, limesema shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO. Taarifa ya Flora Nducha Inafafanua

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa shirika hilo mwaka jana umefungana na mwaka 2007 kama miaka inayoshika nafasi ya sita yenye joto kali ardhini na baharini ikiwa na nyuzi joto 0.50C sawa 0.90F ikiwa juu ya wastani wa kiwangio cha joto kuanzia 1961-1990 miaka iliyokuwa na wastan wa nyuzi joto 0.03C au 0.05F.

Kiwango hicho cha mwaka jana kimepita pia rekod ya miaka ya karibuni ya 2001 hadi 2010.Miaka inayoshikilia rekodi ya juu hadi sasa ni 2005 na 2010 ikifuatiwa na mwaka 1998 ambao mbali ya joto kali ulighubikwa na zahma ya El Nino. Michele Garraud ni Mkurugenzi Mkuu wa WMO

(SAUTI YA MICHELLE GARRAUD)

"mwaka 2013 utashika nafasi ya sita kwenye rekodi ya miaka yenye joto kali saana katika historia tangu karne ya 19.Na hii ni thibitosho kwamba ongezeko la joto linaendelea tunaona kwamba ingawa joto linaongezeka lakini sio sawia kila mahali kuna sehemu zimevunja rekodi ya joto kali mfano Australia mwaka 2013 umeweka rekodi ya joto kali saana kuwahi kushuhudiwa katika nchi hiyo. Ni muhimu saana tukiongelea ongezeko la joto tusijikite tuu katika sehemu ndogo ya dunia bali tuangalie na mambo mengine ."