Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CERF yatenga dola Milioni 86 kusaidia nchi 10 zenye majanga mabaya zaidi.

CERF yatenga dola Milioni 86 kusaidia nchi 10 zenye majanga mabaya zaidi.

Mratibu Mkuu wa usaidizi wa kibinadamu ndani ya Umoja  wa Mataiaf Valerie Amos ametenga dola Milioni 86 kwa ajili ya operesheni za usaidizi za Umoja huo kwenye maeneo yenye majanga makubwa zaidi na ambayo pia yamesahaulika.

Fedha hizo zinatoka mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia majanga, CERF na zinaelekezwa nchi kumi ambazo ni Mali, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, Uganda, Colombia, Haiti, Myanmar, Djibouti, Sudan na Yemen, ambako mahitaji ni makubwa lakini fedha hakuna.

Bi. Amos amesema majanga kwenye maeneo hayo yamesahaulika kutokana na kuibuka kwa mizozo mingine akiweka bayana kuwa dola Milioni 11.5 zitaelekezwa Mali ambako bado watu wanahama kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya mwaka 2012 yaliyosababisha wengi kupoteza makazi.

Mwaka 2006 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianzisha mfuko huo wa dharura ili kurahisisha usaidizi kwa maeneo yenye dharura na kuweka uwiano. Tangu kuanzishwa kwake CERF inayopata fedha kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na wahisani imeshatoa zaidi ya dola Bilioni 3.2 kwa mashirika ya usaidizi wa kibinamu kwenye nchi 88 na maeneo.