Kampeni kimataifa dhidi ya bidhaa bandia yazinduliwa: UNODC

14 Januari 2014

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti w madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC imezindua kampeni mpya ya kimataifa ya kuibua uelewa juu ya madhara  ya usafirishaji haramu wa bidhaa bandia.

Kampeni hii kupitia matangazo ya umma inaitwa, Bandia, usinunue na kutumbukia kwenye uhalifu wa kupangwa, na ina lengo la kuelimisha wanunuzi wa bidhaa hizo kuwa fedha zitokanazo na bidhaa husika zinaweza kutumika kuendesha vikundi vya uhalifu, kuathiri afya ya mtumiaji au hata kusababisha uharibifu wa mazingira.

Bidhaa hizo ni pamoja na vifaa vya teknolojia ya kisasakamavile simu, matairi ya magari, dawa za binadammu na hata wanyama, nguo na hata mabegi.  Pierre Lapaque mwakilishi wa ofisi ya UNODC kanda ya Afrika Magharibi na Kati na katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa amesema mwelekeo wa biashara hiyo si mzuri.

Miongoni mwa dawa bandia zilizotajwa kutumbukia kwenye mtego huo ni pamoja na zile za kupungumza maumivu, kuondoa uzio, kuongeza urijali na hata kutibu saratani na kupunguza uzito. UNODC inasema biashara haramu ya dawa bandia kutoka Asia Mashariki na Pasifiki kwenda nchi zaAsiaya Kusini-Mashariki na  barani Afrika inafikia dola bilioni Tano kwa mwaka.