Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka rasilimali zitumike kuimarisha amani

UM wataka rasilimali zitumike kuimarisha amani

Ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa vyombo vya kidola, serikali, mashirika ya kiserikali na washirika wengine wanawajibu wa kuongeza nguvu ili kuoanisha rasilimali zilizopo na kuwa tunu mpya ya uletaji amani kwenye maeneo yaliyokumbwa na mizozo.

Ripoti hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho nafasi ya rasilimali kwenye ujenzi mpya wa jamii iliyokumbwa na mzozo imezinduliwa leo Mjini New York na kusisitiza haja ya mashirikiano.

Imesema kuwa rasilimali zinazokutikana kwenye maeneo yaliyokumbwa na machafuko zinaweza kugeuzwa na kutumikakamadaraja jipya la uletaji upatanisho na amani ya kudumu.

Ripoti hiyo pia imesema kuwa rasilimalikamamadini, gesi na mafuta zinahitaji kusimamiwa vyema ili kuhakikisha kwamba zinasaidia vyakutosha kwenye ujenzi wa jamii mpya.