Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani na UM wazindia mpango kufadhili kilimo

Marekani na UM wazindia mpango kufadhili kilimo

Kundi moja la Umoja wa Mataifa linalounga mkono maendeleo vijijini pamoja na serikali ya Marekani wamezindua mpango wa kuziwesesha jamii za wahamiaji kuwekeza kwenye kilimo kwenye nchi wanakotoka.

Mpango huo uliozinduliwa mjini Washington utashiriakia na na wahamiaji walio na nia ya kuwekeza kwenye miradi ya kilimo kwenye jamii wanakotoa hasa nchi ambazo zimekubwa na mizozo awali.

Rais wa shirika la kutoa ufadhili wa maendeleo ya kilimo la Umoja wa Mataifa IFAD Kanayo Nwanze anasema kuwa jamii zinazoishi ngambo huwa zinawekeza jumla ya dola bilioni 400 kila mwaka na nyingi zingetaka kusaidia nchi zao.

Huku zaidi ya watu milioni 215 au asilimia 3 ya watu wote duniani wakiishi nchi za kigeni jamii hizo tayari zimetoa mchango mkubwa wa kiuchumi kwa nchi nyingi.