Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Karibu nusu ya dunia watakabiliwa na upungufu wa maji 2030:

Karibu nusu ya dunia watakabiliwa na upungufu wa maji 2030:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema kudhibiti rasilimali muhimu ya maji ni changamoto hasa kutokana na ongezeko la uchafusi wa mazingira na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.Flora Nducha na taarifa kamili

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa maji na usafi mjini Budapest Hungary amesema ifikapo mwaka 2030 karibu nusu ya watu wote duniani watakabiliwa na upungufu wa maji huku mahitaji yakizidi upatikanaji kwa rakribani asilimia 40.

Ban amesema kuna ushindani mkubwa hivi sasa miongoni mwa sekta ya viwanda na kilimo, mijini na vijijini na changamoto zinazojitokeza ni suala la dunia nzima na sio mtu au sekta moja.Ameongeza kuwa jinsi ya kushughulikia changamoto hizo itakuwa muhimu saana katika mustakhbali wa dubnia kwani maji ni nguzo muhimu katika maendeleo

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

“Tunayahitaji kwa afya, usalama wa chakula na maendeleo ya kiuchumi. Lakini kila mwaka yanaleta shinikizo jipya. Maji yanapotea na kutumika vibaya na sekta zote katika nchi zote. Hii inammanisha kwamba sekta zote katika nchi zote lazima kushirikiana kwa suluhu endelevu. Ni lazima tutumie tulichonacho vyema na kwa umakini”

Baadaye Ban amekutana na Rais wa Hungary na kasha khutubia chuo kikuu cha Corvinus ambako ametunukiwa shahada ya heshima ya uzamuivu, (Phd)