Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado kuna mkwamo ndani ya Baraza la usalama kuhusu Syria: Balozi Quinland

Bado kuna mkwamo ndani ya Baraza la usalama kuhusu Syria: Balozi Quinland

Mpango kazi wa mwezi Septemba kwa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa chini ya uongozi wa Australia umeonyesha kuwa suala la Mashariki ya Kati hususan Syria litaendelea kuangaziwa. Mpango kazi huo umewasilishwa kwa waandishi wa habari na Mwakilishi wa kudumu waAustraliakwenye umoja wa mataifa Balozi Gary Quinlan. Amesema kadri siku zinavyosonga watu wengi wanashangaa kwa kasi ya kupatia suluhu suala hilo lakini kubwa ni mkwamo wa mazungumzo ndani ya baraza hilo hususan miongoni mwa wajumbe muhimu. Amesema hata hii leo wajumbe walipatiwa muhtasari wa ziara ya Mkuu wa siasa ndani ya Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman huko Mashariki ya Kati alikojadili hatma ya suluhu kwa Syria na wakati hata baada ya mashauriano ya faragha bado kuna mkwamo na kwa sasa mkutano wa G20 unaanza Urusi, hata kama Syria siyo ajenda bado itachukua nafasi kubwa.

 (Sauti ya Quinlan)

 “Ukweli ni kwamba mwelekeo sasa ni huko kujaribu kuona iwapo kuna uwezekano wa kuondokana na mkwamo.nafikiri wengi wameona kwamba kwa sasa kuwa na kikao cha baraza la usalama juu ya hilo haitazaa matunda yoyote. Tumejadili asubuhi hii kwa mapana kuhusu mashariki ya kati,hakuna mabadiliko yoyote, na iko bayana kuwa tushughulikia suala hilo kwa ngazi ya viongozi wa juu zaidi,kuona iwapo inaweza kupata suluhisho katika G20.”

Ratiba ya mpango kazi inaonyesha kuwa tarehe 26 mwezi huu kutakuwepo na kikao cha ngazi ya juu cha kujadili silaha ndogondogo na tishio lake kwa amani na usalama duniani ambapo Balozi Quinlan amesema kuna uwezekano kwa mara ya kwanza wakapitisha azimio