FAO yazindua vitabu vyake vya kwanza vya mtandao

24 Julai 2013

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa  FAO limezindua vitabu vyake vya kwanza vya mtandao vinavyoanganzia masuala kadha  kuhusu chakula , kilimo na vita dhidi ya njaa. Jason Nyakundi anaripoti(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kwa sasa nakala za kwanza za vitabu hivyo vinapatikana bila malipo  kwenye wavuti wa Shirika la FAO. Nakala zingine zaidi zinatarajiwa kuwekwa kwenye mtandao kwenye awamu ambayo itaendela hadi baadaye mwaka  huu kabla ya vitabu hivyo kuanza kupatika kwenye hifadhi zingine za vitabu.

Naibu mkuu kwenye kitengo cha uchapishaji katika Shirika la FAO Rachel Tucker anasema kuwa vitabu hivyo vikiwa vinaangazia masuala teule kwa njia ya mtandao ni hatua iliyo muhimu.

Anasema kuwa FAO ina habari nyingi kuhusu chakula, kilimo na njia za kupambana na njaa yote ambayo  yatapatikana kwa urahisi kwa wale wanaoyahitaji. Vitabu hivyo vyote vianapatikana kwa lugha ya kiingereza.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter