Liberia yahitaji dola Milioni 37 kukidhi mahitaji ya kibinadamu 2013

19 Februari 2013

Serikali ya Liberia na Umoja wa Mataifa hii leo wametangaza ombi la dola Milioni 37 zitakazotumika kukidhi mahitaji ya binadamu nchini humo kwa mwaka huu wa 2013 kutokana na hali ngumu inayoendelea kukabili wananchi.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari kuwa Liberia inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu ambapo takribani nusu ya wananchi ni mafukara wakitumia chini ya dola moja kwa siku kukidhi maisha yao huku kukiwa na jukumu la wakimbizi

(SAUTI YA Martin)

“Zaidi ya wakimbizi Elfu Sitini na Wanne wa Ivory Coast bado wanaishi Liberia tangu wakimbie vurugu zilizotoka na uchaguzi nchini mwao, na wakimbizi wa zamani Elfu Ishirini na watano wa Liberia waliorejea nchini mwao nao bado wanahitaji misaada muhimu ya kibinadamu.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter