Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usaidizi wa dharura umeongezeka na kuuweka UM kwenye majaribio: OCHA

Usaidizi wa dharura umeongezeka na kuuweka UM kwenye majaribio: OCHA

Idadi kubwa ya watu ambayo haijawahi kutokea wanaanza mwaka mpya wakiwa ni wakimbizi wa ndani au wamekimbilia nchi jirani na hivyo kuwa ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Mataifa kwenye utoaji usaidizi wa kibinadamu.

Hiyo ni kauli ya Mkuu wa masuala ya usaidizi wa kibinadamu ndani ya umoja wa Mataifa Valerie Amos aliyotoa mjiniNew York, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Ametaja mzozo wa Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati naSyriaambayo kila uchao inasababisha maelfu ya watu kuacha makaziyaona kusaka misaada ilhali wenginekamavile Ufilipino wakikumbwa na majanga ya asili.

(Sauti ya Amos)

 “Mwaka 2013 ulikuwa jaribio halisi la mfumo wa usaidizi wa binadamu duniani, na  hakuna dalili yoyote ya mabadiliko mwaka 2014. Ni dhahiri kuwa Umoja wa Mataifa na wadau wake wanahitajika zaidi. Upana na ugumu wa mazingira ya dharura niliyotaja vitaendelea kutoa changamoto kwa mfumo wa utoaji misaada ya kibinadamu duniani ”

Halikadhalika Bi. Amos amezungumzia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huko Sudan Kusini,Syria, Jamhuri ya Afrika ya Kati na kwingineko kwenye mizozo ambapo amesema hali hiyo inafanya ajenda ya Umoja wa Mataifa kuhusu  haki za binadamu kuendelea kuwa na umuhimu zaidi wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.