Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awapa hongera Wamisri kwa miaka miwili tangu mapinduzi

Ban awapa hongera Wamisri kwa miaka miwili tangu mapinduzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amepeleka salamu za heko kwa raia wa Misri, wakati wakiadhimisha miaka miwili tangu mapinduzi yaloing’oa serikali ya Hosni Mubarak mamlakani.  Bwana Ban ameelezea kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kuwaunga mkono watu wa Misri na serikali yao kujenga mifumo ya kidemokrasia inayowahusisha wote.

Amewahimiza waendelee kushabikia kanuni za kimataifa za mazungumzo ya amani na kuepukana na ghasia, uhusishaji wa wote, heshima ya haki za binadamu, uhuru wa taasisi za serikali na misingi ya demokrasia ambayo inaruhusu dhana tofauti. Amehimiza pia umuhimu wa kuwahusisha wanawake katika kufanya maamuzi muhimu.