Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yahofia usalama wa wafilipino waliobakia Syria

IOM yahofia usalama wa wafilipino waliobakia Syria

Usalama wa raia wa Ufilipino ambao bado wamebakia Syria baada ya wenzao kuanza kurejea makwao unatia hofu shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM.

Mratibu wa IOM nchini Syria Othman Belbesi amesema kuwa idadi kubwa ya raia hao wameshindwa kuondoka kutokana  na kutojua namna watavyoondoka. Baadhi yao wanadaiwa kukwama katika maeneo ambayo siyo salama kwa maisha yao.

Wengine inasemekana wamekosa nyaraka muhimu za kuondokea hivyo wameendelea kusota bila msaada wowote. Idadi kubwa wamekuwa wakifanya kazi za ndani nchini Syria kwa kipindi kirefu cha hadi miaka 30.

IOM inakadiria kuwa wafilipino kati ya 120,000 hadi 150,000 wanahitaji msaada wa kuondolewa nchini Syria na kurejeshwa nyumbani.