Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubaliano ya Geneva bado msingi wa amani Syria: Brahimi

Makubaliano ya Geneva bado msingi wa amani Syria: Brahimi

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi ametoa muhtasari wa mazungumzo yake na naibu mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani  William Burns na yule wa Urusi Mikhail Bogdanov yaliyofanyika huko Geneva, Uswisi ambapo amesema kwa pamoja wametambua madhila wanayopata wananchi wa Syria na kwamba suluhisho la amani ndio njia pekee ya mzozo huo.

Amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva.

(SAUTI YA Brahimi)

Halikadhalika amesema wamekubaliana nyaraka ya Geneva kuhusu mwelekeo wa Syria ndio msingi wa suluhu la mzozo huo na kutaka wajumbe wa Baraza la Usalama kuweka fursa ya kutatua mgogoro wa Syria.

Bwana Brahimi pia amesema kuwa kamwe hajawahi kusema kuwa chombo kitakachoongoza Syria wakati wa mpito hakitajumuisha wajumbe wa serikali ya sasa.