Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna njia ya mkato kwa suluhu ya Israel na Palestina:Obama

Hakuna njia ya mkato kwa suluhu ya Israel na Palestina:Obama

Rais Barack Obama wa Marekani amesema hakuna njia ya mkato ya kufikia suluhu ya amani baina ya Israel na Palestina. Akizungumza kwenye mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Obama amesema amani inategemea kuafikiana miongoni mwa watu ambao ni lazima waishi pamoja baada ya kumalizika kwa hotuba na kura kuhesabiwa.

Amesema hilo ndio somo lililopatikana Ireland ya Kaskazini, Sudan ambako majadiliano yamesababisha kuundwa kwa taifa jipya na hiyo ndio njia ya kupita kufikia taifa la Palestina huo ndio ukweli wenyewe, kwani kila upande una haki ya matarajio na hivyo kufanya suala la amani kwa ngumu. Lakini ameongeza

(SAUTI YA BARACK OBAMA)

Mkwamo huo wa amani utaondolewa tu ambapo kila upande utajifunza kubeba machungu ya mwingine, hilo ndilo tulichagize. Chombo hili kilichoanzishwa kutokana na majivu ya vita na mauaji ya kimbari lazima kitambue ukweli ulioko baina ya Israel na Palestina. Hatua zetu lazima ziangalie endapo zinasukuma mbele haki za watoto wa Israel au Palestina kuishi pamoja kwa amani na usalama. Tutafanikiwa tu katika juhudi hizo endapo tutazishawishi pande hizo kuketi, kusikilizana na kuelewa hofu na matumaini ya kila upande na ho ndio mradi ambao Marekani imejikita na hilo ndiolo Umoja wa mataifa unapaswa kulifanyia kazi katika wiki na miezi ijayo.