Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumaliza migogoro vijana lazima wawezeshwe:Kagame

Kumaliza migogoro vijana lazima wawezeshwe:Kagame

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema ili kumaliza migogoro na vita vinavyoisonga dunia ni lazima kuyawezesha makundi muhimu katika jamii ikiwemo vijana.

Akizungumza kwenye mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Rais Kagame amesema dunia itapaswa kuangalia kwa makini chanzo cha watu kufarakana na kutaka kufaidika na kuwa na maisha bora duniani, jambo ambalo litaongeza uwezo wa kukabiliana na migogoro hiyo.

Amesema kuwa kushughulikia masala muhimu ya maendeleo kwa mfano kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia dunia itajenga mazingira bora ya kuwa na dunia imara isiyo na machafuko.

(SAUTI YA RAIS KAGAME)