Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la UM limezitaka nchi wanachama kuadhimisha siku ya amani kwa njia bora

Baraza Kuu la UM limezitaka nchi wanachama kuadhimisha siku ya amani kwa njia bora

Azimio namba 55/282 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limezitaka nchi wanachama na mashirika duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani kwa njia muafaka kupitia shughuli mbalimbali zikiwemo kuelimisha jamii, kuimarisha malengo ya amani na kumaliza mivutano na migogoro.

Akitoa ujumbe maalumu katika siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 21 mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa ni kuchagiza amani na maridhiano Somalia. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)