Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brazil inaendelea kuunga mkono kazi ya UM kuinua wanawake na kutimiza MDG's

Brazil inaendelea kuunga mkono kazi ya UM kuinua wanawake na kutimiza MDG's

Rais wa Brazil Dilma Rosseff amesema nchi yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na Umoja wa Mataifa kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa. 

Akizungumza kwenye mjada wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bi Rosseff ambaye ni mwanamke wa kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa kuwa wa kwanza kuhutubia baraza hilo amegusia masuala mbalimbali ikiwemo mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa utakaofanyika Juni 2012, kutokomeza umasikini, kuwawezesha wanawake, kutimiza haki za binadamu, kuleta usawa na kikubwa zaidi kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015. 

(SAUTI YA DILMA ROUSSEFF)