Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma ya afya karibu watu huboresha ufanisi na imani: WHO

Huduma ya afya karibu watu huboresha ufanisi na imani: WHO

Licha ya juhudi za jumuiya ya kimataifa kuhakikisha watu hupata huduma za afya karibu na wanakoishi, shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kwamba takwimu zinaonyesha mtu mmoja kati ya 20 hawapati huduma za afya muhimu zinazoweza kutolewa katika  kiliniki badala ya hospitali.

Katika ujumbe wake unaofafanuliwa kwa njia ya video, WHO imesema kwenye wavuti wake kwamba inaunga mkono hatua za bima duniani kwa kubuni afya kwa watu badala ya vituo vya magonjwa au afya.

Hatua hiyo itasaidia watu kupata huduma sahihi, kwa wakati muafaka na sehemu sahihi, imesema WHO na kuongeza kuwa watu huishi na hali zao za kiafya saa 24, sio tu wanapohitaji huduma.

Kwa kuboresha huduma za afya kuwa karibu na watu huongeza imani, kujiamiani na hata wahudumu wa afya hupata utoshelevu pamoja na mfumo mzima kuwa bora na fanisi.